Back to top

Marufuku wanafunzi kuchapwa viboko Kenya.

07 February 2022
Share

Waziri wa Elimu nchini Kenya George Magoha awaonya walimu dhidi ya kuwachapa viboko wanafunzi na kuwakumbusha watu kwamba adhabu ya viboko bado ni marufuku katika shule za nchi hiyo.

Waziri  Magoha amesema walimu watakaobainika kuwapiga wanafunzi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Kauli yake inajiri siku chache baada ya mwanafunzi kupigwa kwa sababu ya kula chapati tano ikiwa ni zaidi ya zile ambazo walikuwa wamepangiwa kula.