
Waziri wa katiba na sheria Mhe.George Simbachawene ameitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kuhakikisha inafikisha elimu kwa jamii kuhusu shughuli za tume hiyo ambapo kumekuwepo na changamoto ya jamii kuripoti polisi matukio ambayo yanatakiwa kushughulikiwa na tume hiyo.
Mhe.Simbachawene ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati wa ziara ya kutembelea ofisi ya tume hiyo na kupokea ripoti ya utendaji kazi watume hiyo na kuiagiza kujenga utaratibu wa kutembelea maeneo mbalimbali ya kijamii ili kuona hali yahaki za wananchi.
Awali Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora Jaji Mstaafu Methew Mwaimu amesema tume tayari imeanza kufanya uchunguzi wa kina juu ya mauaji yanayoendelea hapa nchini kwa sasa miongoni mwa jamii.
