
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bi. Jokate Mwegelo amesema kufuatia kuungua moto kwa soko la Mbagala Rangitatu, wameunda Kamati ya Uchunguzi wa chanzo cha moto huo huku akibainisha kuwa wametoa siku tatu hadi nne kwa Kamati hiyo kukamilisha uchunguzi wake ambapo pia wametoa maelekezo kwa Manispaa kuwaruhusu wafanyabiashara kurudi Sokoni pale uchunguzi utakapokuwa umekamilika.
