Back to top

Wahamiaji haramu 45 wakamatwa Dodoma.

13 February 2022
Share

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limewakamata wahamiaji haramu 45 raia wa Ethiopia ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Polisi Onesmo Lyanga amesema kuwa wahamiaji hao wana umri wa kati ya miaka 15 hadi 21 na walikamatwa katika eneo la Mlima Kolo wilayani Kondoa wakiwa safarini kuelekea mataifa ya kusini mwa Afrika.