
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ambaye ni mshtakiwa wa kesi ya ugaidi amevunja ukimya katika vizimba vya Mahakama kuu divisheni ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi baada ya kunyoosha mkono na kuifahamisha Mahakama hiyo kuwa hawapewi chakula gerezani kwa muda wa miezi mitano sasa ambapo mshtakiwa huyo alibainisha kuwa hata pale kesi inapoahirishwa mchana kwa mapumziko kwa ajili ya kupata chakula wao hawapati chakula wala maji kwa miezi yote hiyo na wakifika gerezani wanakuta wenzao wameshakula.
