Back to top

Simba SC yamsamehe Bernard Morrison.

14 February 2022
Share

Klabu ya Simba imetoa taarifa ya kumsamehe mchezaji wake Bernard Morrison baada ya kumsimamisha na kumpa siku 7 za kuandika barua na kueleza kwanini asichukuliwe hatua zaidi za kinidhamu kufuatia tuhuma zinazomkabili za utovu wa nidhamu, ambapo mchezaji huyo aliandika barua hiyo na kuomba radhi kwa CEO wa Simba SC Barbara Gonzalez, Kocha Pablo Franco na benchi la ufundi kwa ujumla huku akiahidi kutorudia tena makosa hayo.