Back to top

Ummy: Acheni matumizi holela ya P2.

15 February 2022
Share

Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu amewataka wasichana na wanawake kuacha matumizi holela ya vidonge vya kuzuia mimba (P2) kwa sababu zinaweza kusababisha ugumba na saratani, Waziri Ummy aeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram, akiwa anatoa elimu juu ya matumizi ya vidonge hivyo vya kuzuia mimba ambavyo hutumika pale msichana ama mwanamke anapokuwa amebakwa, kondom kupasuka na kwa wale waliokosea hesabu za siku zao hedhi ili kuepuka kutoa mimba (Abortion) au kuzaa watoto wasiotarajiwa.
.
Amebainisha kuwa kama serikali wanatambua kuna matumizi yasio sahihi ya dawa hizo hasa kwa watoto wa shule ambao kwa sasa inaonekana wanaogopa zaidi mimba kuliko UKIMWI, ameeleza kuhusu hatua ambazo wanaendelea kuzijadili ndani ya serikali ikiwa ni kuongeza kasi ya utoaji elimu juu ya madhara ya matumizi holela ya P2 ambapo ameshailelekeza timu yake kushughulikia hilo.