Back to top

Watu 46 wafariki ndani ya miezi 6 mkoani Geita

17 February 2022
Share

Jeshi la Polisi mkoani Geita limesema jumla ya watu 46 wamefariki katika kipindi cha miezi sita mkoani humo ambapo Jeshi hilo limebainisha kuwa watu 28 kati yao wamefariki kwa kujinyonga kutokana na msongo wa mawazo huku 18 wakiuawa kutokana na imani za kishirikina, hali iliyopelekea Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo Henry Mwaibambe kuwaomba viongozi wa dini kusaidia kutoa elimu kwenye nyumba za ibada ili kupunguza mauaji.