
Meli tatu zinazosafirisha abiria na mizigo mikoa ya Mbeya, Ruvuma na Njombe pamoja na nchi ya Malawi kupitia Ziwa Nyasa zimeharibika na kupaki katika bandari ya Kiwira Wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Meli ya abiria ya Mbeya Two ilipata hitilafu Januari 1 mwaka huu na meli mbili za mizigo za MV.Njombe na MV.Iringa hazifanyi kazi kwa muda mrefu huku MV.Njombe imefanya safari moja toka itengenezwe ambapo mhandisi na nahodha wa meli ya MV.Mbeya wanazungumzia hitilafu ya meli hiyo.
Meneja wa bandari ya Ziwa Nyasa Bw.Abdala Mohamed anaeleza hatua zinazochukuliwa kuitengeneza meli ya MV.Mbeya Two baada ya uchunguzi wa maofisa wa bima.
