Back to top

Auawa na kuchomwa moto kwa kujaribu kubaka

25 February 2022
Share

Mwanaume mmoja ambaye jina lake halijafahamika ameuawa kwa kupigwa kisha kuchomwa moto na wananchi wa eneo la Bombambili mkoani Geita akidaiwa kumteka na kujaribu kumbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16 alfajiri wakati akielekea shuleni ambapo Kamanda wa Polisi mkoani humo Henry Mwaibambe amebainisha kuwa wanamshikilia Kiongozi wa Serikali katika eneo hilo huku msako wa kuwakamata wananchi waliojichukulia sheria mkononi ukiendelea.