Back to top

Mwanafunzi alieandika barua kuacha shule alikosa chakula.

25 February 2022
Share

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Msimbati, Wilayani Mtwara Mkoani Mtwara Taufiq Salum Hamis aliyeandika barua ya kuacha shule amekubali kurudi kuendelea na masomo baada ya kudai alikuwa akikosa chakula na vifaa vya shule ambapo amejitokeza mdau kumsaidia mahitaji yake na kisha kupatiwa ushauri ili aendelee na masomo.
.
Feb 24 mwanafunzi huyo alimuandikia barua Mkuu wa Shule hiyo, Hamis Sadala ya kukataa Shule huku akisema hana nia mbaya na wala hajashinikizwa na Mtu bali amefanya uamuzi huo ili apate nafasi nzuri ya kufanya shughuli za uvuvi kwenye maeneo anayoishi.