
Wizara ya Mambo ya Nje imetoa taarifa kuhusu hali ya Watanzania walioko nchini Ukraine ambapo Wizara hiyo imebainisha kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua za haraka ili Watanzania takribani 300 waliopo nchini humo kuondoka na kuingia katika nchi za Poland na Romania ambako kuna utulivu ili kuwawezesha kurejea nchini kwa usalama.

