
Mkuu wa Wilaya ya Hanang Janet Mayanja ameagiza kukamatwa kwa waganga wa kienyeji wasiokuwa na vibali vya serikali na wale wanaopiga ramli chonganishi kwa kutembea nyumba kwa nyumba maarufu kama Lamba Lamba na kupelekea taharuki na uvunjifu wa amani baada ya waganga hao kuwatuhumu baadhi ya watu kujihusisha na ushirikina.
