Back to top

Tanzania kuendeleza ushirikiano na AU

28 February 2022
Share

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema Tanzania itaendelea kuunga mkono na kuimarisha ushirikiano uliopo na Umoja wa Afrika hasa katika kuzingatia misingi ya haki za binadamu na utawala bora, demokrasia na utawala wa sheria.
.
Waziri Mkuu ameyasema hayo alipomuwakilisha Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa mkutano wa 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu unaofanyika jijini Arusha.