
Jeshi la Urusi limedai kuwa vikosi vyake vya kijeshi vimepiga vituo 1,146 vya kijeshi vya Ukraine tangu kuanza kwa operesheni yake maalum nchini Ukraine ambapo Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi, Meja Jenerali Igor Konashenkov amebainisha kuwa malengo yalikuwa ni vituo 31 vya amri, vituo vya mawasiliano, mifumo ya kombora ya ndege pamoja na vituo 75 vya rada na wanajeshi wameendelea kusonga mbele katika mikoa yote miwili inayounga mkono Moscow mashariki mwa Ukraine.
