
Katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita, shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwemo mikutano ya Waheshimiwa Mawaziri na Vyombo vya Habari itayoanzia tarehe 1 – 16 Machi, 2022 ili kueleza utekelezaji wa Serikali ikiwemo miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali kwa kipindi cha mwaka mmoja. Pia, Wizara na Taasisi za Serikali zitashiriki vipindi mbalimbali vya Redio na Televisheni.

