
Wizara ya ulinzi ya Urusi imetoa taarifa ya onyo kwa wakazi wa Kyiv kuwa vikosi vyake vinajiandaa kufanya mashambulizi katika maeneo maalum katika mji mkuu wa Ukraine, ambapo imebainisha kuwa maeneo yaliyolengwa ni vituo vya kiteknolojia vya huduma ya usalama ya Ukraine na kituo kikuu cha 72 cha PsyOps huku Maafisa hao wakidai kuwa mashambulizi hayo yanafanywa ili kuzuia mashambulizi ya mawasiliano dhidi ya Urusi.
