Back to top

NAPE ASEMA SERIKALI HAIJAKATAA KUKOSOLEWA.

10 March 2022
Share

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Nape Nnauye amesema kuwa serikali haikatai kukosolewa na vyombo vya habari ila inachokataa ni namna ya ukosoaji ambao hauna afya kwa taifa.

"Kama nakukosoa kwa namna ya kukudhalilisha hata kama ukosoaji wangu una maana lakini nikiweka udhalilishaji juu yake inapoteza maana yake, kwa hiyo mimi nadhani suala sio ukosoaji suala ni unakosoaje"

Akizungumza kwenye kipindi cha DAKIKA 45 kinachorushwa na ITV Mhe.Nape amesema kama ukosoaji unalenga kuivunjia heshima serikali ukosoaji huo hauwezi kukubalika, lakini ikiwa ukosoaji huo ni kwa nia ya kujenga hakuna mtu atakaye kasirika na ikitokea atakaye kasirika basi ana matatizo.

"Serikali zinaongozwa na wanasiasa tunajifunza kuwa na ngozi ngumu sana kwa sababu tunakopitia, mi mbunge unaweza ukaenda sehemu ukakuta mtoto anakutukana lakini ukiwa mwanasiasa unajifunza kuvumilia kwa sababu ndio sampuli ya watu unayokutana nayo …serikali iko tayari kuambiwa madhaifu na tunaheshimu vyombo vya habari ni jicho letu’alisemw Waziri Nape.

Amefafanua kwamba Rais Samia amesema mara kadhaa vyombo vya habari  vinamsaidia kufichua maovu, ndio maana kunakuwa  na habari za uchunguzi.

"Mimi kama Waziri wa Habari,ni maelekezo ya Rais kwamba tuikosoe serikali kadri tunavyoweza isipokuwa tuikosoe kwa staha…tusiikosoe kwa kudhalilisha, unataka kumsema Nape kakosea mseme kwa heshima usisahau kwamba na yeye ni binadamu"