Back to top

Vivutio vya Utalii vya Tanzania kutangazwa LALIGA

11 March 2022
Share

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amefanya mazungumzo na Uongozi wa vilabu vya Atletico Madrid na Getafe vinavyoshiriki Ligi Kuu ya Hispania (Laliga) kwa lengo la kuitangaza Tanzania hususani sekta ya utalii ambapo baada ya mazungumzo hayo Waziri Ndumbaro alisema viongozi wote wa vilabu wameonesha utayari wa kushirikiana katika kuitangaza Tanzania kiutalii kupitia matangazo kwenye jezi za Vilabu pamoja na mbao za matangazo (billboards) zilizopo uwanjani.

Aidha, Dkt.Ndumbaro amefanya mazungumzo na Klabu ya Real Valladolid inayomilikiwa na mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa Brazil, Ronaldo De Lima ambapo Klabu hiyo inatarajia kupanda daraja kushiriki Laliga.

"Shabaha yetu kubwa kama nchi ni kuhakikisha tunafungamanisha utalii na michezo kwa kutumia timu kubwa za mpira kwa lengo la kuwavutia watalii wengi zaidi kuja nchini Tanzania" alisisitiza Dkt.Ndumbaro