Back to top

SAMIA ATOA MAAGIZO UANDAAJI KANUNI MIKUTANO VYAMA VYA SIASA

12 March 2022
Share

Rais Samia amuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. Balozi Dokta Pindi Chana kuandaa kanuni zitakazoelekeza namna ya kufanya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

Rais Samia ametoa maelekezo hayo baada ya kupokea maazimio ya awali kutoka Kikosi kazi alichokiteua cha kufuatilia hoja zilizojitokeza katika mkutano wa wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa uliofanyika jijini Dodoma Desemba 15 hadi 17 mwaka 2021.

Rais Samia amemwagiza Waziri huyo wa Katiba na Sheria kushirikiana na Tanganyika Law Society (TLS) pamoja na Zanzibar Law Society (ZLS) kutengeneza kanuni hizo.

Kikosi kazi hicho chenye wajumbe 24, na ambacho kinawajibika moja kwa moja kwa Mhe. Rais, kiliwasilisha maazimio hayo Ikulu Jijini Dodoma.

Maazimio hayo yamegawanyika katika makundi matatu ya muda wa utekelezaji.