
Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Jenista Mhagama ameagiza kufanyika ukaguzi wa matumizi ya fedha zaidi ya shilingi bilioni 41 ambazo serikali ilitoa kwa halmashauri zilizopitiwa na mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania Mkurabita ili kuhakikisha fedha hizo zimeleta tija kwa wanyonge.
Mhe.Mhagama ametoa maagizo hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na watumishi wa Mkurabita ambapo amesisitiza mfumo wa urasimishaji ardhi na biashara uendelee kusimamiwa ili uweze kuleta tija kwa Watanzania hususani wanyonge.
Aidha Mhe.Mhagama amewaagiza watendaji wa Mkurabita kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa masijala za ardhi na kuzikabithi katika ofisi za vijiji kabla ya Juni 30 mwaka huu.
