Back to top

Serikali: Mfumuko wa bei, sio uzembe ni majanga

15 March 2022
Share

Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha kwa wananchi hakusababishwi na tatizo la kisera wala uzembe bali unatokana na uwepo wa majanga yanayoendelea kuikumba dunia.
.
Dkt. Mwigulu ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya Habari akieleza utendaji na mafanikio ya serikali ya awamu ya sita katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan.