Back to top

Wanaoiba dawa za serikali waondolewe.

16 March 2022
Share

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Philip Mpango  ameagiza watumishi wa sekta ya afya katika zahanati, vituo vya afya na hospitali watakaobainika kushiriki katika wizi wa dawa za serikali waondolewe kazini mara moja . 

Akizungumza na wakazi wa kata ya Bagara  mkoani Manyara Dk.Philip Mpango amesema kuwa serikali haitawavulimia watumishi wa sekta ya afya wanaoiba dawa za serikali. 

kwa upande wake Naibu Waziri wa TAMISEMI David Silinde amesema kuwa serikali  itahakikisha upatikanaji wa dawa pamoja na kudhibiti upotevu wa dawa.