Back to top

UJENZI WA BANDARI YA UVUVI MBIONI KUANZA

16 March 2022
Share


Serikali imeweka wazi kuwa mradi wa ujenzi wa bandari ya uvuvi unatarajia kuanza muda wowote kuanzia sasa baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu. Bandari ambayo inatarajiwa kujengwa Wilayani Kilwa Masoko, Mkoani Lindi inatarajiwa kuwa chachu ya kuimarika kwa uchumi wa buluu nchini.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Utafiti na Mafunzo ya uvuvi, Dkt. Erastus Mosha wakati wa mkutano wa wadau uliolenga kupitia rasimu ya taarifa ya upembuzi yakinifu wa mradi huo wa kimkakati uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Dkt.Mosha ameeleza kuwa bandari hiyo itaiwezesha nchi kupata mapato kupitia meli za uvuvi na bidhaa zinazotokana na uvuvi zitauzwa hapa ndani na nje ya nchi.

Ameongeza kuwa Serikali tayari imetenga fedha za kufanikisha ujenzi huo ambao unatarajiwa kufanyika katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia sasa.