Back to top

Hatua za utoaji elimu ya ufugaji kwa wanafunzi mbioni.

20 March 2022
Share

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema serikali itaanza hatua za utoaji elimu ya ufugaji kwa wanafunzi kwa kuanzisha Klabu zitakazowajengea uwezo wa ufugaji na kuwapatia ajira hata baada ya kumaliza masomo yao.

Amesema hayo katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya kukusanyia na kusindika bidhaa za maziwa kwa vyama vya ushirika wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

Alisema Klabu hizo za kutoa elimu ya ufugaji wa aina mbalimbali za mifugo zitaanzishwa hasa kwenye shule zenye maeneo makubwa ili wanafunzi wapate eneo la kutosha kwa ufugaji