
Balozi wa China nchini Marekani Qin Gang amesema kuwa nchi hiyo haitatuma silaha kusaidia vita vya Urusi nchini Ukraine na kwamba China "itafanya kila kitu ili kupunguza mzozo".
.
Balozi Gang amesema hayo baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kumuonya mwenzake wa China Xi Jinping siku ya Ijumaa kwamba kutakuwa na "matokeo" ikiwa China itatoa msaada wa kijeshi kwa Moscow.
