
Jeshi la Ukraine limesema Urusi imeongeza zana za kijeshi katika anga la Ukraine huku likibainisha kuwa mbali na matumizi ya ndege nyingi zisizo na rubani, Urusi inatumia vilipuzi, ndege za kivita, makombora ya kivita, na makombora ya balestiki ambapo Jeshi hilo siku ya Jumatatu lilifanikiwa kuharibu ndege, helikopta mbili na ndege zisizo na rubani sita za Urusi, madai ambayo bado hayajathibitishwa.
