
Mahakama ya Rufani Tanzania, Masjala ya Iringa imeondoa kesi iliyokuwa inamkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania, Abdul Nondo ambaye alikuwa anashtakiwa kwa kosa la kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni na kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma Mafinga ambapo leo Machi 23, 2022, kesi hiyo ilikuwa inafika mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa lakini Wakili wa Serikali, Basilius Namkambe aliwasilisha ombi katika mahakama hiyo kuwa DPP hana nia ya kuendelea na keshi hiyo.
