
Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema ikiwa unataka gesi ya nchi hiyo lazima utumie sarafu ya Urusi(Ruble) kwa nchi zote zisizo rafiki wa nchi hiyo zikiwemo nchi za Umoja wa Ulaya (EU) ambapo muda mfupi baada ya uamzi huo sarafu hiyo iliyoshuka thamani kutokana na vikwazo vilivyowekwa kwa nchi hiyo imeimarika dhidi ya dola na Euro.
