
Maafisa wa serikali ya Ukraine wamesema kuwa shehena ya makombora 1,500 ya kutungulia ndege aina ya Strela na bunduki 100 za MG3 zimewasili nchini humo kutoka nchini Ujerumani.
.
Ujerumani imebatilisha sera yake ya kihistoria ya kutopeleka silaha katika maeneo yenye mizozo kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
