Back to top

Rais Dk. Mwinyi ampongeza Tony Blair.

27 March 2022
Share

Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi amempongeza Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Tony Blair  kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi zake za kuendelea kuiunga mkono Zanzibar hasa katika mipango na mikakati ya upangaji wa vipaumbele kwa watendaji wa Serikali.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo wakati alipofanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Tony Blair Ikulu Zanzibar ambaye yupo Zanzibar kwa ziara maalum.

Katika maelezo yake Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Waziri Mkuu Mstaafu Tony Blair kupitia taasisi yake ya (Tony Blair Institute for Global Change), imeweza kuunga mkono jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kutoa mafunzo kwa watendaji wakuu juu ya upangaji wa vipaumbele hatua ambayo ina umuhumu mkubwa katika mipango ya Serikali.

Nae Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Tony Blair Ikulu Zanzibar alimueleza Rais Dk. Mwinyi hatua zinazoendelea kuchukuliwa na taasisi yake katika kuhakikisha malengo na mikakati ya kuiunga mkono Zanzibar yanatekelezeka na kuzaa matunda.