
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba ametoa ushauri kwa mtu yeyote anayekwenda kwenye mazungumzo na Urusi "asile au kunywa chochote, na ikiwezekana kuepuka kugusa sehemu yoyote".
.
Ushauri huo unafuatia baada ya Bilionea wa Urusi Roman Abramovich na wapatanishi wengine wa Ukraine kudaiwa kuwekewa sumu mapema mwezi huu katika mazungumzo ya amani kwenye mpaka wa Ukraine na Belarus.
