
Wadau wa sekta ya maji mkoani Shinyanga wameishauri serikali kuanza utaratibu wa kuweka maofisa wa maji katika kila kata kama ilivyo katika sekta zingine kama kilimo na afya ili kutatua changamoto ya wananchi kupata majisafi na salama huku wakiomba kodi iondolewe kwenye vipuli na viunganishio vya mabomba ya maji kwa lengo la kuvifanya vipatikane kupunguza adha ya wananchi kushindwa kujiunganishia maji.
Kauli hiyo imetolewa na wadau wa sekta ya maji mkoani Shinyanga katika kikao kazi cha kubadili changamoto zinazokwamisha upatikanaji wa majisafi na salama kwa wananchi kilichoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na kutoa misaada ya kibinadamu kwa wananchi wanaoishi katika maeneo yenye changamoto ya ukame na upatikanaji wa maji la TCRS kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society.
Mhandisi wa Maji Ofisi ya RUWASA mkoa wa Shinyanga amesema kuwa ushauri wa wadau ameuchukua kuupeleka mahali husika.
