Back to top

Serikali kusimamia sera za lishe nchini

01 April 2022
Share

Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Bajeti Ofisi ya Waziri Mkuu  Bw. Eleuter Kihwele amesema Serikali itaendelea kuratibu na kusimamia sera zinazohusu masuala ya lishe kama hatua ya kukabiliana na utapiamlo na udumavu ndani ya jamii ili kuhakikisha inakuwa salama na yenye afya bora. 


Aidha, Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa Lishe ni suala mtambuka linalohusisha wadau wote na wananchi hasa katika muktadha mzima wa kubadili tabia ya ulaji wa vyakula unaozingatia misingi ya lishe hivyo kuwe na mpango wa miaka mitano ambao utakuwa ni rahisi kueleweka kwa wananchi na kutekeleza.