
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Bw. Kaspar Mmuya amewataka wananchi kuepuka kujenga katika maeneo hatarishi yanayoweza kusababisha maafa kama vifo, uharibifu wa miundo mbinu na mazingira nchini ambapo amebainisha kuwa ipo haja ya wananchi kupewa elimu kupitia wataalamu mbalimbali kuhusu dhana ya usimamizi wa maafa na namna ya kuzuia madhara ya maafa au kuchukua hatua ya kujiokoa pindi yanapotokea.

Aidha, Bw.Kaspar Mmuya amezungumza kuhusu hali ya hewa ambapo amewahimiza wakulima nchini kuzingatia utabiri wa hali ya hewa ambao umekuwa ukitolewa na wataalam ili kujua mazao rafiki ya kulima kwa msimu husika.
.
“Tuangalie mabadiliko ya hali ya hewa tuweze kulima kulingana na hali ya hewa na elimu hii itatolewa kwa wakulima kama kipindi cha mvua nyingi tunatakiwa kulima nini na wakati wa mvua chache tulime nini elimu hii itatolewa maneo yote,” alieleza.
