
Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro amesema moja ya mikakati ya Jeshi la Polisi kanda hiyo ni kuzuia biashara ya Wanawake kujiuza kwa kuwakamata Wanaume ambao wanahusika katika biashara hiyo ambapo amebainisha kuwa ameamua kuja na staili tofauti ambayo haitahusisha matumizi ya nguvu kwa Wanawake wanaofanya biashara hiyo.
