Back to top

Mbaroni kwa kuharibu miundombinu ya reli

05 April 2022
Share

Jeshi la Polisi kikosi cha TAZARA limemkamata Juma Makondo Mutula (49) mkazi wa kibaoni Kisarawe na wenzake watatu kwa tuhuma kuharibu miundombinu ya reli kwa kufungua vyuma vinavyounganisha reli, baada ya operesheni maalum iliyofanyika kwa kipindi cha tarehe 1 – 31, Machi 2022 ambapo baada ya upekuzi katika nyumba za watuhumiwa hao walikutwa na vyuma vya reli ya TAZARA na baadhi ya alama za barabarani. 
.
Hata hivyo, Baada ya mahojiano ya kina watuhumiwa hao walibainisha kuwa vyuma hivyo walitaka kuviuza kama vyuma chakavu na wote watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kwa hatua zaidi.