Back to top

Serikali yafanya malipo ya ndege tano mpya

06 April 2022
Share

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imeendelea kuliimarisha Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ili liweze kutoa huduma bora ya usafiri wa anga ndani na nje ya nchi ambapo amebainisha kuwa serikali imefanya malipo ya awali ya ununuzi wa ndege tano mpya kati ya hizo, ndege moja ni aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, ndege mbili aina ya Boeing 737-9, ndege moja aina ya De Havilland Dash 8-Q400, na ndege moja ya mizigo aina ya Boeing 767-300F hivyo kuifanya serikali kuwa na jumla ya ndege mpya 16.