Back to top

MILANGO IPO WAZI MWENYE TAARIFA UNAFUU WA MAFUTA

13 April 2022
Share

Waziri wa Nishati Mhe.Janury Makamba amesema endapo kuna mtu yeyote mwenye taarifa za kusaidia nchi kuleta mafuta ya bei nafuu basi milango ipo wazi anamkaribishwa ofisini kwake kwa mazungumzo, kuliko kung'ang'ana na bei ya juu kumbe kuna uwezekano wa kupata unafuu kwenye bidhaa hiyo kwani nchi hii ni ya watu wote. 

Kauli ya Waziri Makamba ameitoa Bungeni Dodoma ambapo amewahakikishia Watanzania kuwa mafuta yapo ya kutosha kulinganisha na nchi jirani.

"Niwahakikishie Watanzania kwa nchi yetu ukilinganisha na majirani zetu, mafuta ya kutosha yapo juu ya kiwango cha kanuni tulizoweka ya siku 15, mafuta yapo na serikali itahakikisha yanaendelea kuwepo ili uchumi usisimame".

Kwa sasa mafuta na bidhaa mbalimbali zimekuwa bei juu kwa kile kinachoelezwa kuwa vita kati ya Ukraine na Urusi ndio husababisha mfumuko huo wa bei kila kona.