
Kuelekea Sikukuu ya Pasaka Jeshi la Polisi nchini limesema limejiimarisha kwa kushirikiana na viongozi wa dini hususani kamati za ulinzi katika nyumba za ibada ili kuhakikisha ibada na sherehe za Pasaka zinafanyika katika mazingira ya amani, utulivu na usalama.
.
Aidha, Jeshi hilo limewatakia watanzania wote heri ya Pasaka yenye upendo, furaha, amani, utulivu na mshikamano huku likiwaomba viongozi wa dini, waumini na watanzania kwa ujumla ushirikiano wa kuendelea kuelimishana na kukemea maovu ndani ya jamii.
