
Naibu Waziri Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe.David Silinde amesema serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 10 katika mwaka wa fedha 2022/23 kwa ajili matengezo ya kipande cha barabara ya Kakonko mkoani Kigoma chenye urefu wa Kilomita 5 kutoka Guarama hadi Mlange ili kuhakikisha huduma za kiuchumi na Kijamii kwa wananchi zinaendelea kufanyika.
Mhe.Silinde amesema hayo wakati Kipindi Cha maswali na majibu akijibu swali la Mbunge wa Buyungu Aloyce Kamamba kuhusu uboreshaji wa barabara ya Kakonko ambayo inasimamiwa na Mamlaka mbili ya TARURA na TANROADS.
Silinde amesema serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya barabara za jimbo Hilo kwa mujibu wa upatikanaji wa fedha.
Aidha akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Buyungu, Aloyce Kamamba kuhusu kuhamishwa kwa Msimamizi wa kipande cha barabara hiyo kutoka TARURA kwenda TANROADS kutokana na umuhimu wa barabara hiyo kuunganisha mataifa ya Burundi na Tanzania Mhe.Silinde amesema wamelipokea jambo hilo na endapo itakidhi vigezo wataioandisha hadhi.
