
Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na kuzungumza na Balozi wa India katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Binaya Srikanta Pradhan, Ikulu Zanzibar ambapo amepongeza juhudi zinazochukuliwa na Ubalozi wa India nchini Tanzania kwa kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miradi mikubwa ya maji safi na salama.
