Back to top

WAZIRI BASHUNGWA AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MVOMERO

20 April 2022
Share

Waziri wa TAMISEMI, Mhe.Innocent Bashungwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro, Hassani Njama Hassani ili kupisha uchunguzi. Waziri Bashungwa amechukua hatua hiyo baada ya Mkurugenzi huyo kushindwa kutekeleza maagizo aliyoyatoa wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya wilayani hapo Machi 10, 2022.

Kwenye taarifa ya TAMISEMI kwa waandishi wa habari imeeleza kuwa Wakati wa ziara ya Waziri Bashungwa alibaini upotevu wa Fedha za miradi na matumizi yasiyo sahihi ya kiasi cha shilingi milioni 231.84 katika ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Moringe Sokoine zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa bwalo la chakula, jiko na bweni na kumuagiza Mkurugenzi huyo kuwachukulia hatua za kiutumishi Wakuu wote wa Idara na watumishi waliohusika na ukiukwaji wa taratibu za manunuzi katika mradi huo.

Hassani Njama Hassani - Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero aliyetumbuliwa.

Maamuzi ya kusimamishwa kazi yanakuja kuwa hadi leo hakuna Mkuu wa Idara yeyote ama Mtumishi aliyechukuliwa hatua kufuatia maagizo ya Waziri Bashungwa.