
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema Serikali imeandaa mashindano ya Insha kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari nchi nzima (Tanzania Bara na Zanzibar) yatakayofanyika kuanzia ngazi ya Shule hadi Mkoa ambapo hadi sasa yamefikia ngazi ya mikoa.
.
Mhe. George Simbachawene ameyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari Mjini Dodoma akielezea maandalizi ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinazotarajiwa kufanyika Aprili 26, mwaka huu.
