Back to top

Wami kukamilika kabla ya muda uliopangwa

21 April 2022
Share

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa Daraja jipya la Wami lenye urefu wa mita 513.5 na barabara za maingilio zenye urefu wa KM 3.8, unatarajiwa kuandika historia kubwa kwa kukamilika kabla ya muda uliopangwa kwenye mkataba ambapo ujenzi huo ulianza mwezi Oktoba, 2018 na unatarajiwa kukamilika mapema ifikapo mwezi Julai, 2022 badala ya mwezi Novemba kama ilivyo kwa mujibu wa mkataba wake.