
Naibu Katibu Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw.Kaspar Mmuya amesema serikali itaendelea kusimamia uandaaji wa bajeti unaozingatia masuala ya kijinsia kama sehemu ya mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa.

Bw.Mmuya ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya Uandaaji wa Bajeti zinazozingatia Usawa wa Kijinsia ili kuwajengea uwezo wakurugenzi na wakuu wa witengo kutoka ofisi hiyo yaliyofanyika Dodoma.
