Back to top

Bil.5 za vikundi vya wanawake zachukuliwa Mwanza

22 April 2022
Share

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel ameagiza watumishi wote wa Umma katika Mkoa huo waliochukua pesa zaidi ya shilingi bilioni tano za vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu kuchukuliwa hatua za kisheria na kusimamishiwa mishahara yao huku akiwataka walioidhinisha kutoka kwa fedha hizo watafutwe popote walipo na warudishwe mkoani humo ili nao wachukuliwe hatua.