
Katibu Mkuu wa CCM, Bw.Daniel Chongolo amewataka wananchi wasipotoshwe na Wanasiasa kuhusiana na suala la Bodaboda na Bajaji katika jiji la Dar es Salaam, ambapo amewahakikishia madereva na watumiaji wa usafiri huo kwamba hawawezi kuondolewa kati kati ya Jiji.
Baada ya kukutana na viongozi wa CCM pamoja na Watendaji wa serikali Wilaya ya Ilala akiwemo Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya hiyo Bw.Chongolo amebainisha hayo na kuleza kuwa zoezi linaloendelea Dar es Salaam ni kuwapanga wenye Bajaji na Bodaboda.
Chongolo amesema Bodaboda na Bajaji ni watu muhimu ambao wanajitafutia kipato hivyo hawawezi kuwaondoa na kuwataka watu kuacha kutoa taarifa za upotoshaji kwa Umma.

Amebainisha waendesha Bajaji baadhi yao ni watu wenye ulemavu, ambao ni kundi maalum linalopata mikopo inayotolewa na Halmashauri 10% hivyo lazima waheshimiwe kwa kuwaweka eneo maalum ili wasigombanie abiria na watu wengie wasiokua na ulemavu.
Kadhalika Katibu Mkuu Chongolo ametumia mkutano huo kuwakumbusha majukumu wajumbe wa kamati za siasa za ngazi zote wakiwemo viongozi wa Jumuiya ambapo kwa sasa kwa tathimini iliyopo Kamati hizo hazitekelezi majukimu sawasawa hasa kusimamia ajenda za wananchi.
