
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe.Ummy Nderiananga wakati akiwasilisha msimamo Tanzania katika mkutano wa dharura wa Kamati ya Mawaziri wanaohusika na Usimamizi wa Maafa uliofanyika kwa njia ya mtandao nakueleza kwamba serikali imeridhia mkataba wa uanzishwaji wa kituo hicho.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe.Ummy Nderiananga wakati akiwasilisha msimamo Tanzania katika mkutano wa dhararua wa Kamati ya Mawaziri wanaohusika na Usimamizi wa Maafa uliofanyika kwa njia ya mtandao nakueleza kwamba serikali imeridhia mkataba wa uanzishwaji wa kituo hicho.
Ameeleza kuwa la kuanzisha kituo hicho ni kusimamia masuala ya maafa na huduma za kibinadamu kwa Nchi Wanachama zitakazokumbwa na maafa hivyo kitasaidia kuendeleza ushirikiano, kuimarisha uwezo wa Kikanda wa kukabiliana na maafa pamoja na kujenga mazingira rafiki ya shughuli za maendeleo hatimaye kukuza uchumi wa Jumuiya.
"Sisi kama Nchi tumeridhia mkataba huo na tunaipongeza serikali ya Msumbiji kwa kukubali kijengwe katika nchi yao na sisi tutaendelea kushirikiana kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha kinafanya kazi na kutoa taarifa na takwimu katika Ukanda wa Afrika na hata kutoa misaada ya kibinadamu wakati wa majanga"Asema.Mhe.Ummy.
Amebainisha kwamba serikali ya Tanzania imekubali ombi la msaada wa kibinadamu kwa Nchi ya Afrika Kusini inayohitaji kiasi cha fedha dola za Kimarekeni 300,000 kufuatia majanga ya mafuriko yalitokea nchini humo huku akiomba sekretarieti kuendelea kufuata utaratibu wa utoaji wa fedha hizo ili kusaidia manusura hao.
"Serikali imeunga mkono kuhusu ombi la msaada kwa Jamhuri ya Afrika Kusini kutokana na mafuriko waliyoyapata kule upande wa Kwazulu Nata sisi kama serikali tumeridhia jambo hilo na kuendelea kushauri sekretarieti ifuate utaratibu wa utoaji wa fedha hizo"Amefanua Mhe.Ummy.


