Back to top

WHO yaripoti maambukizi mapya ya Ebola Congo

24 April 2022
Share

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kisa kimoja cha mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, Kaskazini Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo Shirika hilo limebainisha kuwa mgonjwa aliyekutwa na maambukizi hayo alionesha dalili siku ya Aprili 5 lakini hakufanya jitihada ya kupata matibabu kwa zaidi ya wiki moja na baadaye alilazwa katika kituo cha matibabu ya Ebola na alifariki siku hiyohiyo.
.
Mlipuko wa mwisho kutokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ulihusisha pia eneo la mashariki ambao ulisababisha maambukizi ya Watu 11 kati ya Oktoba na Desemba na kuwaua sita.